watanzania tuelimishane: ndio njia moja ya maendeleo!
Kama kweli tunataka maendeleo ya nchi na wananchi basi lazima tuipe serikali fulsa ya kufanya kazi yake. Tujaribu kutoa ushauri au mapendekezo ya jinsi maswala ya maendelo yata sululishwa. Kazi hii sio rahisi kwa serkali yeyote leo ni CCM kesho labda ni CHADEMA au chama kingine chochote na yvama vyote hivi vitakutana na matatizo tofauti megine mapya na magine ya kurithi.
Sasa ni mfumo gani upinzania utachukua? Matatizo ya Tanzania sio ni kwa sababu tu ya viongozi fulani fulani kuto kuangali nyuma au kwenye kio cha kuangalia nyuma wakati wanaendesha, au kula bila ya kuona haya, ni pia yanasababisha na hali ya kiuchumi duniani (bei za mafuta nk, garama za usafirishaji etc), ukosefu wa washauri ambao wanaweza kuona mbali, kwa upeo na upana au picha halisi.
Matatizo pia ni kwamba Tanzania inashindwa kushinda katika soko la dunia kwa sababu infrastructure yetu bado hafifu na pia bado tunatumia teknoligia ya zamani na bado ni wachanga katika kuweza kujiuza na kijupromote nje, elimu, umme, korruption, ujuzi wa masoko ya nje na jinsi wenzetu wanavyo fanya biashara, etc etc.
Maswala ni mengi na yote haya yanachangia katika kutokutesheleza haja za watu hasa wenzetu wa hali ambayo sio nzuri. Kuto kuweza kuwa na msimamo na plani au strategia katika maswala kwenye bodi kama WTO. Haya yote yanachangia. Sasa kama kunaupinzani unaopenda maendeleo ni kuanza kuangalia maswala kama haya na kuweka wazi pamoja ya kupiga darubini serkali inafanya nini. Badala ya kuweka vikwazo ni vizuri kushirikiana katika matatizo kwani kila siku inayo pita Tanzania tunaptoteza fedha na umasikini kuzidi na wenje uwezo wa kujisaidia kwamanufaa yao wenyewe serikalini kuendelea.
Tusisahau kwamba kuna success stories nyingi Tanzania hizi lazima zipewe mwanga zaidi. Watanzania lazima tuelimishane kwamba maendeleo yanaletwa pia nakujitegemea wewe binafsi lakini kuwepo na njia ya kuweka hivyo vyombo vya umma ambavyo vitamsaidia mtu wa kawaida kujiwezesha kujitegemea.
Mie kwa kusema ukweli naona serikali inajitahidi sana, na uongozo unajitahidi. Sie tukiwa tunakosoa tu kwajili ya kukosoa bila ya kuleta majibu ya jinsi ya kutatua matatizo basi hatufiki mbali. Ni rahisi kua mpinzani. Tafuteni solution mlio soma, wakilisheni Tanzania katika mabodi tofauti na pia badilisheni picha ya nchi huko mlipo. Tusaidieni sie walalahoi.